Native Bible

Joshua 4:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Basi waambieni, ‘Israeli ilivukia mahali pakavu katika Mto Yordani.’

Joshua 4:22 in English

Joshua 4:22 · Berean Standard Bible

you are to tell them, ‘Israel crossed the Jordan on dry ground.’

Context

20Naye Yoshua akayasimamisha huko Gilgali yale mawe kumi na mawili ambayo walikuwa wameyachukua katikati ya Mto Yordani. 21Akawaambia Waisraeli, “Wazao wenu watakapowauliza baba zao siku zijazo wakisema, ‘Mawe haya maana yake ni nini?’ 22Basi waambieni, ‘Israeli ilivukia mahali pakavu katika Mto Yordani.’ 23Kwa maana Bwana Mungu wenu alikausha maji ya Yordani mbele yenu, hadi mlipomaliza kuvuka. Bwana Mungu wenu alifanya haya kwa Mto Yordani sawasawa na kile alichoifanyia Bahari ya Shamu wakati alipoikausha mbele yetu hadi tulipomaliza kuvuka. 24Alifanya hivi ili kwamba mataifa yote ya dunia yapate kujua kuwa mkono wa Bwana ni wenye nguvu, na ili kwamba kila wakati mpate kumcha Bwana Mungu wenu.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.