Native Bible

Joshua 19:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kuelekea upande wa magharibi ukafika Marala, ukagusa Dabeshethi, na kuendelea mpaka kwenye bonde karibu na Yokneamu.

Joshua 19:11 in English

Joshua 19:11 · Berean Standard Bible

It went up westward to Maralah, reached Dabbesheth, and met the brook east of Jokneam.

Context

9Urithi wa Wasimeoni ulitolewa kutoka fungu la Yuda, kwa kuwa fungu la Yuda lilikuwa kubwa kuliko walivyohitaji. Hivyo kabila la Simeoni lilipewa urithi wao ndani ya eneo la Yuda. 10Kura ya tatu ikaangukia kabila la Zabuloni, ukoo kwa ukoo: Mpaka wa urithi wao uliendelea hadi Saridi. 11Kuelekea upande wa magharibi ukafika Marala, ukagusa Dabeshethi, na kuendelea mpaka kwenye bonde karibu na Yokneamu. 12Ukageuka mashariki, kuanzia Saridi kuelekea mawio ya jua hadi kwenye nchi ya Kisiloth-Tabori, na kwenda hadi Daberathi, kupanda Yafia. 13Kisha ukaendelea mashariki hadi Gath-Heferi na kufika Eth-Kasini, ukatokea Rimoni na kugeuka kuelekea Nea.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.