Native Bible

Joshua 18:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kisha ukaenda mpaka kwenye mteremko wa kaskazini wa Beth-Hogla na kujitokeza kwenye ghuba ya kaskazini ya Bahari ya Chumvi, kwenye maingilio ya Yordani upande wa kusini. Huo ulikuwa mpaka wa kusini.

Joshua 18:19 in English

Joshua 18:19 · Berean Standard Bible

The border continued to the northern slope of Beth-hoglah and came out at the northern bay of the Salt Sea,* at the mouth of the Jordan. This was the southern border.

Context

17Kisha ukapinda kuelekea kaskazini, ukaenda hadi En-Shemeshi na kuendelea mpaka Gelilothi, inayotazamana na Njia ya Adumimu, ukateremka hadi kwenye Jiwe la Bohani mwana wa Reubeni. 18Ukaendelea upande wa mteremko wa kaskazini wa Beth-Araba ukateremka hadi Araba. 19Kisha ukaenda mpaka kwenye mteremko wa kaskazini wa Beth-Hogla na kujitokeza kwenye ghuba ya kaskazini ya Bahari ya Chumvi, kwenye maingilio ya Yordani upande wa kusini. Huo ulikuwa mpaka wa kusini. 20Nayo Yordani ikawa ndio mpaka wa upande wa mashariki. Hii ilikuwa ndiyo mipaka iliyoonyesha urithi wa koo za Benyamini pande zote. 21Kabila ya Benyamini, ukoo kwa ukoo, ilikuwa na miji mikubwa ifuatayo: Yeriko, Beth-Hogla, Emeki-Kesisi,

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.