Yoshua 15:12
Joshua 15:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mpaka wa magharibi ni pwani ya Bahari Kuu. Hii ndiyo mipaka ya watu wa Yuda kwa koo zao.
Joshua 15:12 in English
Joshua 15:12 · Berean Standard Bible
And the western border was the coastline of the Great Sea. These are the boundaries around the clans of the descendants of Judah.
Context
10Kisha ukapinda upande wa magharibi kutoka Baala hadi Mlima Seiri, ukafuatia sambamba mteremko wa kaskazini mwa Mlima Yearimu (yaani Kesaloni), ukaendelea chini hadi Beth-Shemeshi na kukatiza hadi Timna. 11Ukaelekea hadi kwenye mteremko wa kaskazini mwa Ekroni, ukageuka kuelekea Shikeroni, ukapita hadi Mlima Baala na kufika Yabineeli. Mpaka ule ukaishia baharini. 12Mpaka wa magharibi ni pwani ya Bahari Kuu.
Hii ndiyo mipaka ya watu wa Yuda kwa koo zao. 13Kwa kufuata maagizo ya Bwana kwake, Yoshua alimpa Kalebu mwana wa Yefune sehemu katika Yuda: Kiriath-Arba, yaani Hebroni (Arba alikuwa baba wa zamani wa Anaki). 14Kutoka Hebroni Kalebu alifukuza hao wana watatu wa Anaki, nao ni Sheshai, Ahimani na Talmai, wazao wa Anaki.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.