Yoshua 12:4
Joshua 12:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nayo nchi ya Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa mmoja wa mabaki ya Warefai, aliyetawala Ashtarothi na Edrei.
Joshua 12:4 in English
Joshua 12:4 · Berean Standard Bible
And Og king of Bashan,* one of the remnant of the Rephaim, who lived in Ashtaroth and Edrei.
Context
2Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni.
Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ilijumlisha nusu ya Gileadi. 3Pia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethi* hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi*), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya materemko ya Pisga. 4Nayo nchi ya Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa mmoja wa mabaki ya Warefai, aliyetawala Ashtarothi na Edrei. 5Naye alitawala katika Mlima Hermoni, Saleka, Bashani yote hadi mpaka wa watu wa Geshuri, na watu wa Maaka na nusu ya Gileadi, hadi kwenye mpaka wa Sihoni mfalme wa Heshboni. 6Mose, mtumishi wa Bwana, na Waisraeli wakawashinda. Naye Mose mtumishi wa Bwana akawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.