Native Bible

Joshua 10:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Baada ya Yoshua kutembea usiku kucha kutoka Gilgali, akawashambulia ghafula.

Joshua 10:9 in English

Joshua 10:9 · Berean Standard Bible

After marching all night from Gilgal, Joshua caught them by surprise.

Context

7Basi Yoshua akaondoka Gilgali pamoja na jeshi lake lote, wakiwepo watu wote mashujaa wa vita. 8Bwana akamwambia Yoshua, “Usiwaogope watu hao, nimewatia mkononi mwako. Hakuna yeyote atakayeweza kushindana nawe.” 9Baada ya Yoshua kutembea usiku kucha kutoka Gilgali, akawashambulia ghafula. 10Bwana akawafadhaisha mbele ya Waisraeli, nao wakawashinda kwa ushindi mkuu huko Gibeoni. Israeli wakawafukuza kuelekea njia iendayo Beth-Horoni wakiwaua mpaka kufikia njia iendayo Azeka na Makeda. 11Walipokuwa wakikimbia mbele ya Israeli kwenye barabara iteremkayo kutoka Beth-Horoni hadi Azeka, Bwana akawavumishia mawe makubwa ya mvua kutoka mbinguni, na wengi wao wakauawa na hayo mawe kuliko wale waliouawa kwa upanga wa Waisraeli.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.