Native Bible

Jonah 3:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Siku ya kwanza, Yona aliingia mjini. Akatangaza: “Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa.”

Jonah 3:4 in English

Jonah 3:4 · Berean Standard Bible

On the first day of his journey, Jonah set out into the city and proclaimed, “Forty more days and Nineveh will be overturned!”

Context

2“Ondoka uende katika mji mkubwa wa Ninawi, ukautangazie ujumbe ninaokupa.” 3Yona akalitii neno la Bwana naye akaenda Ninawi. Basi Ninawi ulikuwa mji maarufu sana, ilichukua siku tatu kuuzunguka. 4Siku ya kwanza, Yona aliingia mjini. Akatangaza: “Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa.” 5Watu wa Ninawi wakamwamini Mungu, wakatangaza kufunga, watu wote kuanzia mkubwa sana hadi yule mdogo kabisa, wakavaa nguo za gunia. 6Habari zilipomfikia mfalme wa Ninawi, aliondoka kwenye kiti chake cha enzi, akavua majoho yake ya kifalme, akajifunika nguo ya gunia kisha akaketi chini mavumbini.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.