Yoeli 3:15
Joel 3:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Jua na mwezi vitatiwa giza, na nyota hazitatoa mwanga wake tena.
Joel 3:15 in English
Joel 3:15 · Berean Standard Bible
The sun and moon will grow dark, and the stars will no longer shine.
Context
13Tia mundu,
kwa kuwa mavuno yamekomaa.
Njooni, mkanyage zabibu,
kwa kuwa shinikizo la kukamua zabibu limejaa
na mapipa yanafurika:
kwa kuwa uovu wao ni mkubwa!” 14Umati mkubwa, umati mkubwa
katika bonde la uamuzi!
Kwa kuwa siku ya Bwana ni karibu
katika bonde la uamuzi. 15Jua na mwezi vitatiwa giza,
na nyota hazitatoa mwanga wake tena. 16Bwana atanguruma kutoka Sayuni
na mshindo wa ngurumo kutoka Yerusalemu;
dunia na mbingu vitatikisika.
Lakini Bwana atakuwa kimbilio la watu wake,
ngome imara kwa ajili ya watu wa Israeli. 17“Ndipo mtakapojua kwamba Mimi, Bwana Mungu wenu,
nakaa Sayuni, mlima wangu mtakatifu.
Yerusalemu utakuwa mtakatifu;
kamwe wageni hawatavamia tena.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.