Yoeli 1:16
Joel 1:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Je, chakula hakikukatiliwa mbali mbele ya macho yetu: furaha na shangwe kutoka nyumba ya Mungu wetu?
Joel 1:16 in English
Joel 1:16 · Berean Standard Bible
Has not the food been cut off before our very eyes— joy and gladness from the house of our God?
Context
14Tangazeni saumu takatifu;
liiteni kusanyiko takatifu.
Iteni wazee
na wote waishio katika nchi
waende katika nyumba ya Bwana Mungu wenu,
wakamlilie Bwana. 15Ole kwa siku hiyo!
Kwa kuwa siku ya Bwana iko karibu;
itakuja kama uharibifu
kutoka kwa Mwenyezi.* 16Je, chakula hakikukatiliwa mbali
mbele ya macho yetu:
furaha na shangwe
kutoka nyumba ya Mungu wetu? 17Mbegu zinakauka
chini ya mabonge ya udongo.
Ghala zimeachwa katika uharibifu,
ghala za nafaka zimebomolewa,
kwa maana hakuna nafaka. 18Jinsi gani ngʼombe wanavyolia!
Makundi ya mifugo yanahangaika
kwa sababu hawana malisho;
hata makundi ya kondoo yanateseka.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.