Ayubu 30:2
Job 30:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nguvu za mikono yao zingekuwa na faida gani kwangu, kwa kuwa nguvu zao zilikuwa zimewaishia?
Job 30:2 in English
Job 30:2 · Berean Standard Bible
What use to me was the strength of their hands, since their vigor had left them?
Context
1“Lakini sasa watu wadogo kwa umri kuniliko wananidhihaki,
watu ambao baba zao ningekataa kwa dharau
kuwaweka pamoja na mbwa wangu wa kulinda kondoo. 2Nguvu za mikono yao zingekuwa na faida gani kwangu,
kwa kuwa nguvu zao zilikuwa zimewaishia? 3Wakiwa wamekonda kutokana na kupungukiwa na kwa njaa,
walizurura usiku katika nchi kame iliyo ukiwa. 4Katika vichaka walikusanya mimea ya chumvi,
nacho chakula chao kilikuwa mizizi ya mti wa mfagio.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.