Native Bible

Job 29:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Waliningojea kama manyunyu ya mvua na kuyapokea maneno yangu kama ardhi inyonyavyo mvua ya vuli.

Job 29:23 in English

Job 29:23 · Berean Standard Bible

They waited for me as for rain and drank in my words like spring showers.

Context

21“Watu walinisikiliza kwa tumaini, wakingojea ushauri wangu kwa utulivu. 22Baada ya mimi kuzungumza, hawakusema zaidi; maneno yangu yaliingia masikioni mwao kwa makini. 23Waliningojea kama manyunyu ya mvua na kuyapokea maneno yangu kama ardhi inyonyavyo mvua ya vuli. 24Walipokata tamaa niliwaonyesha uso wa furaha; nuru ya uso wangu ilikuwa ya thamani kwao. 25Niliwachagulia njia na kukaa kama mkuu wao; niliishi kama mfalme katikati ya majeshi yake; nikawa kama yeye anayewafariji waombolezaji.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.