Ayubu 2:9
Job 2:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mke wake akamwambia, “Je, bado unashikamana na uadilifu wako? Mlaani Mungu nawe ukafe!”
Job 2:9 in English
Job 2:9 · Berean Standard Bible
Then Job’s wife said to him, “Do you still retain your integrity? Curse * God and die!”
Context
7Basi Shetani akatoka mbele za Bwana naye akampiga Ayubu kwa majipu mabaya tangu nyayo za miguu yake hadi utosi wa kichwa. 8Ndipo Ayubu akachukua kigae na kujikuna nacho huku akiketi kwenye majivu. 9Mke wake akamwambia, “Je, bado unashikamana na uadilifu wako? Mlaani Mungu nawe ukafe!” 10Akamjibu, “Unazungumza kama vile ambavyo mwanamke mpumbavu* yeyote angenena. Je, tupokee mema mikononi mwa Mungu, nasi tusipokee na udhia?”
Katika mambo haya yote, Ayubu hakutenda dhambi katika kusema kwake. 11Basi marafiki watatu wa Ayubu, ndio Elifazi Mtemani, na Bildadi Mshuhi na Sofari Mnaamathi, waliposikia juu ya taabu yote iliyompata Ayubu, wakajipanga toka manyumbani mwao, nao wakakutana pamoja kwa makubaliano kwenda kumtuliza katika taabu hiyo na kumfariji.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.