Native Bible

Job 1:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Shetani akamjibu Bwana, “Je, Ayubu anamcha Mungu bure?

Job 1:9 in English

Job 1:9 · Berean Standard Bible

Satan answered the LORD, “Does Job fear God for nothing?

Context

7Bwana akamwambia Shetani, “Umetoka wapi?” Shetani akamjibu Bwana, “Natoka kuzunguka pote duniani, nikitembea huku na huko humo.” 8Ndipo Bwana akamwambia Shetani, “Je, umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Hakuna mtu mwingine duniani aliye kama yeye, asiye na hatia, ni mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuepukana na uovu.” 9Shetani akamjibu Bwana, “Je, Ayubu anamcha Mungu bure? 10Je, wewe hukumjengea boma pande zote yeye na wa nyumbani mwake pamoja na kila kitu alicho nacho? Kazi za mikono yake umezibariki na hivyo makundi yake ya kondoo na mbuzi pamoja na ya wanyama yameenea katika nchi nzima. 11Lakini nyoosha mkono wako na kupiga kila kitu alicho nacho, naye kwa hakika atakulaani mbele za uso wako.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.