Yohana 8:43
John 8:43 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa nini hamwelewi ninayowaambia? Ni kwa sababu hamwezi kusikia nisemacho.
John 8:43 in English
John 8:43 · Berean Standard Bible
Why do you not understand what I am saying? It is because you are unable to accept My message.
Context
41Ninyi mnafanya mambo afanyayo baba yenu.”
Wakamjibu, “Sisi hatukuzaliwa kwa uzinzi. Tunaye Baba mmoja, Mungu pekee.” 42Yesu akawaambia, “Kama Mungu angekuwa Baba yenu, mngenipenda, kwa maana nilitoka kwa Mungu na sasa niko hapa. Sikuja kwa ajili yangu mwenyewe, ila yeye alinituma. 43Kwa nini hamwelewi ninayowaambia? Ni kwa sababu hamwezi kusikia nisemacho. 44Ninyi ni watoto wa baba yenu ibilisi, nanyi mnataka kutimiza matakwa ya baba yenu. Yeye alikuwa muuaji tangu mwanzo, wala hakushikana na kweli maana hamna kweli ndani yake. Asemapo uongo husema yaliyo yake mwenyewe kwa maana yeye ni mwongo na baba wa huo uongo. 45Lakini kwa sababu nimewaambia kweli hamkuniamini!
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.