Native Bible

John 8:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hawakuelewa kuwa alikuwa akiwaambia juu ya Baba yake wa Mbinguni.

John 8:27 in English

John 8:27 · Berean Standard Bible

They did not understand that He was telling them about the Father.

Context

25Wakamuuliza, “Wewe ni nani?” Naye Yesu akawajibu, “Mimi ndiye yule ambaye nimekuwa nikiwaambia tangu mwanzo. 26Nina mambo mengi ya kusema juu yenu na mengi ya kuwahukumu. Lakini yeye aliyenituma ni wa kweli, nami nanena na ulimwengu niliyoyasikia kutoka kwake.” 27Hawakuelewa kuwa alikuwa akiwaambia juu ya Baba yake wa Mbinguni. 28Kisha Yesu akawaambia, “Mtakapokwisha kumwinua juu Mwana wa Adamu, ndipo mtakapojua kuwa, ‘Mimi ndiye yule niliyesema na kwamba mimi sitendi jambo lolote peke yangu bali ninasema yale tu ambayo Baba yangu amenifundisha. 29Yeye aliyenituma yu pamoja nami, hajaniacha, kwa kuwa siku zote nafanya mapenzi yake.’ ”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.