Native Bible

John 5:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yesu akamwambia, “Inuka! Chukua mkeka wako na uende.”

John 5:8 in English

John 5:8 · Berean Standard Bible

Then Jesus told him, “Get up, pick up your mat, and walk.”

Context

6Yesu alipomwona akiwa amelala hapo, naye akijua kuwa amekuwa hapo kwa muda mrefu, akamwambia, “Je, wataka kuponywa?” 7Yule mgonjwa akamjibu, “Bwana, mimi sina mtu wa kuniingiza bwawani maji yanapotibuliwa. Nami ninapotaka kutumbukia bwawani, mtu mwingine huingia kabla yangu.” 8Yesu akamwambia, “Inuka! Chukua mkeka wako na uende.” 9Mara yule mtu akapona, akachukua mkeka wake, akaanza kutembea. Basi siku hiyo ilikuwa siku ya Sabato. 10Kwa hiyo Wayahudi wakamwambia yule mtu aliyeponywa, “Leo ni Sabato, si halali wewe kubeba mkeka wako.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.