Native Bible

John 3:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mwili huzaa mwili, lakini Roho huzaa roho.

John 3:6 in English

John 3:6 · Berean Standard Bible

Flesh is born of flesh, but spirit is born of the Spirit.

Context

4Nikodemo akauliza, “Awezaje mtu kuzaliwa wakati akiwa mzee? Hakika hawezi kuingia mara ya pili kwenye tumbo la mama yake ili azaliwe!” 5Yesu akamwambia, “Amin, amin nakuambia, hakuna mtu yeyote anayeweza kuingia Ufalme wa Mungu kama hajazaliwa kwa maji na kwa Roho. 6Mwili huzaa mwili, lakini Roho huzaa roho. 7Kwa hiyo usishangae ninapokuambia huna budi ‘kuzaliwa mara ya pili.’ 8Upepo huvuma popote upendapo. Mvumo wake unausikia lakini huwezi ukafahamu utokako wala uendako. Ndivyo ilivyo kwa kila mtu aliyezaliwa na Roho.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.