Native Bible

John 21:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Baada ya haya Yesu akawatokea tena wanafunzi wake kando ya Bahari ya Tiberia.* Yeye alijionyesha kwao hivi:

John 21:1 in English

John 21:1 · Berean Standard Bible

Later, by the Sea of Tiberias,* Jesus again revealed Himself to the disciples. He made Himself known in this way:

Context

1Baada ya haya Yesu akawatokea tena wanafunzi wake kando ya Bahari ya Tiberia.* Yeye alijionyesha kwao hivi: 2Simoni Petro, Tomaso aitwaye Didimasi, yaani Pacha, Nathanaeli wa Kana ya Galilaya, wana wa Zebedayo na wanafunzi wengine wawili walikuwa pamoja. 3Simoni Petro akawaambia wenzake, “Mimi naenda kuvua samaki.” Nao wakamwambia, “Tutakwenda pamoja nawe.” Wakatoka, wakaingia ndani ya mashua, lakini usiku ule hawakupata chochote.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.