Yohana 19:17
John 19:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
(16) Kwa hiyo askari wakamchukua Yesu. (17) Yesu, akiwa ameubeba msalaba wake, akatoka kuelekea mahali palipoitwa Fuvu la Kichwa (kwa Kiebrania ni Golgotha).
John 19:17 in English
John 19:17 · Berean Standard Bible
Carrying His own cross, He went out to The Place of the Skull, which in Hebrew is called Golgotha.
Context
15Wao wakapiga kelele, “Mwondoe! Mwondoe! Msulubishe!”
Pilato akawauliza, “Je, nimsulubishe mfalme wenu?”
Wale viongozi wa makuhani wakamjibu, “Sisi hatuna mfalme mwingine ila Kaisari.” 16Ndipo Pilato akamkabidhi Yesu kwao ili wamsulubishe. 17(16) Kwa hiyo askari wakamchukua Yesu. (17) Yesu, akiwa ameubeba msalaba wake, akatoka kuelekea mahali palipoitwa Fuvu la Kichwa (kwa Kiebrania ni Golgotha). 18Hapo ndipo walipomsulubisha. Pamoja naye walisulubisha watu wengine wawili, mmoja kila upande wake, naye Yesu katikati. 19Pilato akaamuru tangazo liandikwe na liwekwe juu kwenye msalaba wa Yesu, likasema: “Yesu wa Nazareti, Mfalme wa Wayahudi.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.