Native Bible

John 17:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ninawaombea wao. Mimi siuombei ulimwengu, bali nawaombea wale ulionipa kwa sababu wao ni wako.

John 17:9 in English

John 17:9 · Berean Standard Bible

I ask on their behalf. I do not ask on behalf of the world, but on behalf of those You have given Me; for they are Yours.

Context

7Sasa wamejua ya kuwa vyote ulivyonipa vimetoka kwako, 8kwa kuwa maneno yale ulionipa nimewapa wao, nao wameyapokea na kujua kwamba kweli nimetoka kwako, nao wameamini kuwa wewe ulinituma. 9Ninawaombea wao. Mimi siuombei ulimwengu, bali nawaombea wale ulionipa kwa sababu wao ni wako. 10Wote walio wangu ni wako na walio wako ni wangu, nami nimetukuzwa ndani yao. 11Mimi sasa simo tena ulimwenguni, lakini wao bado wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba Mtakatifu, uwalinde kwa uweza wa jina lako ulilonipa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo wamoja.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.