Yohana 12:3
John 12:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha Maria akachukua chupa ya painti moja* yenye manukato ya nardo* safi ya thamani kubwa, akayamimina miguuni mwa Yesu na kuifuta kwa nywele zake. Nyumba nzima ikajaa harufu nzuri ya manukato.
John 12:3 in English
John 12:3 · Berean Standard Bible
Then Mary took about a pint * of expensive perfume, made of pure nard, and she anointed Jesus’ feet and wiped them with her hair. And the house was filled with the fragrance of the perfume.
Context
1Siku sita kabla ya Pasaka, Yesu alikwenda Bethania mahali ambako Lazaro aliyekuwa amefufuliwa na Yesu alikuwa anaishi. 2Wakaandaa karamu kwa heshima ya Yesu. Martha akawahudumia wakati Lazaro alikuwa miongoni mwa waliokaa mezani pamoja na Yesu. 3Kisha Maria akachukua chupa ya painti moja* yenye manukato ya nardo* safi ya thamani kubwa, akayamimina miguuni mwa Yesu na kuifuta kwa nywele zake. Nyumba nzima ikajaa harufu nzuri ya manukato. 4Ndipo Yuda Iskariote mwana wa Simoni, mmoja wa wale wanafunzi ambaye ndiye angemsaliti Yesu, akasema, 5“Kwa nini manukato haya hayakuuzwa kwa dinari 300* na fedha hizo wakapewa maskini?”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.