Yohana 12:23
John 12:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yesu akawajibu, “Saa imewadia ya Mwana wa Adamu kutukuzwa.
John 12:23 in English
John 12:23 · Berean Standard Bible
But Jesus replied, “The hour has come for the Son of Man to be glorified.
Context
21Hawa wakamjia Filipo, ambaye alikuwa mwenyeji wa Bethsaida huko Galilaya, wakiwa na ombi. Wakamwambia, “Tungependa kumwona Yesu.” 22Filipo akaenda akamweleza Andrea, nao wote wawili wakamwambia Yesu. 23Yesu akawajibu, “Saa imewadia ya Mwana wa Adamu kutukuzwa. 24Amin, amin nawaambia, mbegu ya ngano isipoanguka ardhini na kufa, hubakia kama mbegu peke yake. Lakini ikifa huzaa mbegu nyingi. 25Mtu yeyote anayependa maisha yake atayapoteza, naye ayachukiaye maisha yake katika ulimwengu huu atayaokoa hata kwa uzima wa milele.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.