Yeremia 9:20
Jeremiah 9:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Basi, enyi wanawake, sikieni neno la Bwana; fungueni masikio yenu msikie maneno ya kinywa chake. Wafundisheni binti zenu kuomboleza; fundishaneni kila mmoja na mwenzake maombolezo.
Jeremiah 9:20 in English
Jeremiah 9:20 · Berean Standard Bible
Now, O women, hear the word of the LORD. Open your ears to the word of His mouth. Teach your daughters to wail, and one another to lament.
Context
18Nao waje upesi
na kutuombolezea,
mpaka macho yetu yafurike machozi
na vijito vya maji vitoke kwenye kope zetu. 19Sauti ya kuomboleza imesikika kutoka Sayuni:
‘Tazama jinsi tulivyoangamizwa!
Tazama jinsi aibu yetu ilivyo kubwa!
Ni lazima tuihame nchi yetu
kwa sababu nyumba zetu zimekuwa magofu.’ ” 20Basi, enyi wanawake, sikieni neno la Bwana;
fungueni masikio yenu msikie maneno ya kinywa chake.
Wafundisheni binti zenu kuomboleza;
fundishaneni kila mmoja na mwenzake maombolezo. 21Mauti imeingia ndani kupitia madirishani,
imeingia kwenye majumba yetu ya fahari;
imewakatilia mbali watoto katika barabara
na vijana waume kutoka viwanja vya miji. 22Sema, “Hili ndilo asemalo Bwana:
“ ‘Maiti za wanaume zitalala
kama mavi katika mashamba,
kama malundo ya nafaka nyuma ya mvunaji,
wala hakuna anayekusanya.’ ”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.