Native Bible

Jeremiah 7:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Je, huyaoni hayo wanayoyatenda katika miji ya Yuda na katika barabara za Yerusalemu?

Jeremiah 7:17 in English

Jeremiah 7:17 · Berean Standard Bible

Do you not see what they are doing in the cities of Judah and in the streets of Jerusalem?

Context

15Nitawafukuza mbele yangu, kama nilivyowafanyia ndugu zenu, watu wa Efraimu.’ 16“Kwa hiyo usiombe kwa ajili ya watu hawa, wala usinililie, na usifanye maombi kwa ajili yao; usinisihi, kwa sababu sitakusikiliza. 17Je, huyaoni hayo wanayoyatenda katika miji ya Yuda na katika barabara za Yerusalemu? 18Watoto wanakusanya kuni, baba zao wanawasha moto, na wanawake wanakanda unga na kuoka mikate kwa ajili ya Malkia wa Mbinguni. Wanamimina sadaka za vinywaji kwa miungu mingine ili kunikasirisha. 19Lakini je, mimi ndiye wanayenikasirisha? asema Bwana. Je, hawajiumizi wenyewe na kujiaibisha?

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.