Native Bible

Jeremiah 50:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yeyote aliyewakuta aliwala; adui zao walisema, ‘Sisi hatuna hatia, kwa kuwa wao walitenda dhambi dhidi ya Bwana, malisho yao halisi, Bwana, aliye tumaini la baba zao.’

Jeremiah 50:7 in English

Jeremiah 50:7 · Berean Standard Bible

All who found them devoured them, and their enemies said, ‘We are not guilty, for they have sinned against the LORD, their true pasture, the LORD, the hope of their fathers.’

Context

5Wataiuliza njia iendayo Sayuni na kuelekeza nyuso zao huko. Watakuja na kuambatana na Bwana katika agano la milele ambalo halitasahaulika. 6“Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea; wachungaji wao wamewapotosha na kuwasababisha kuzurura juu ya milima. Walitangatanga juu ya mlima na kilima, na kusahau mahali pao wenyewe pa kupumzikia. 7Yeyote aliyewakuta aliwala; adui zao walisema, ‘Sisi hatuna hatia, kwa kuwa wao walitenda dhambi dhidi ya Bwana, malisho yao halisi, Bwana, aliye tumaini la baba zao.’ 8“Kimbieni kutoka Babeli; ondokeni katika nchi ya Wakaldayo tena kuweni kama mbuzi wale waongozao kundi. 9Kwa maana nitaamsha na kuleta dhidi ya Babeli muungano wa mataifa makubwa kutoka nchi ya kaskazini. Watashika nafasi zao dhidi yake, naye kutokea kaskazini atatekwa. Mishale yao itakuwa kama mishale ya mashujaa walio hodari, ambao hawawezi kurudi mikono mitupu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.