Yeremia 50:1
Jeremiah 50:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hili ndilo neno alilosema Bwana kupitia nabii Yeremia kuhusu Babeli na nchi ya Wakaldayo:
Jeremiah 50:1 in English
Jeremiah 50:1 · Berean Standard Bible
This is the word that the LORD spoke through Jeremiah the prophet concerning Babylon and the land of the Chaldeans:*
Context
1Hili ndilo neno alilosema Bwana kupitia nabii Yeremia kuhusu Babeli na nchi ya Wakaldayo: 2“Tangazeni na mhubiri katikati ya mataifa,
twekeni bendera na mkahubiri;
msiache kitu chochote, bali semeni,
‘Babeli utatekwa;
Beli ataaibishwa,
Merodaki atajazwa na hofu kuu.
Sanamu zake zitaaibishwa
na vinyago vyake vitajazwa hofu kuu.’ 3Taifa kutoka kaskazini litamshambulia,
na kuifanya nchi yake ukiwa.
Hakuna hata mmoja atakayeishi ndani yake,
watu na wanyama wataikimbia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.