Yeremia 5:12
Jeremiah 5:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wamedanganya kuhusu Bwana. Wamesema, “Yeye hatafanya jambo lolote! Hakuna dhara litakalotupata; kamwe hatutaona upanga wala njaa.
Jeremiah 5:12 in English
Jeremiah 5:12 · Berean Standard Bible
They have lied about the LORD and said: “He will not do anything; harm will not come to us; we will not see sword or famine.
Context
10“Piteni katika mashamba yake ya mizabibu na kuyaharibu,
lakini msiangamize kabisa.
Pogoeni matawi yake,
kwa kuwa watu hawa sio wa Bwana. 11Nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda
wamekuwa si waaminifu kwangu kamwe,”
asema Bwana. 12Wamedanganya kuhusu Bwana.
Wamesema, “Yeye hatafanya jambo lolote!
Hakuna dhara litakalotupata;
kamwe hatutaona upanga wala njaa. 13Manabii ni upepo tu, wala neno halimo ndani yao,
kwa hiyo hayo wayasemayo na yatendeke kwao.” 14Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote:
“Kwa sababu watu hawa wamesema maneno haya,
nitayafanya maneno yangu vinywani mwenu kuwa moto,
na watu hawa wawe kuni
zinazoliwa na huo moto.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.