Native Bible

Jeremiah 44:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ndipo Yeremia akawaambia watu wote, wanaume na wanawake waliokuwa wakimjibu,

Jeremiah 44:20 in English

Jeremiah 44:20 · Berean Standard Bible

Then Jeremiah said to all the people, both men and women, who were answering him,

Context

18Lakini tangu tulipoacha kumfukizia uvumba Malkia wa Mbinguni na kummiminia sadaka za kinywaji, hatupati chochote, na tumekuwa tukiangamizwa kwa upanga na njaa.” 19Wanawake wakaongeza kusema, “Wakati tulipomfukizia uvumba Malkia wa Mbinguni na kummiminia sadaka zetu za kinywaji, je, waume zetu hawakujua kwamba tulikuwa tukitengeneza maandazi kwa mfano wake, na kummiminia yeye sadaka za kinywaji?” 20Ndipo Yeremia akawaambia watu wote, wanaume na wanawake waliokuwa wakimjibu, 21“Je, Bwana hakukumbuka na kufikiri juu ya uvumba uliofukizwa katika miji ya Yuda na barabara za Yerusalemu na ninyi pamoja na baba zenu, wafalme wenu, maafisa wenu na watu wa nchi? 22Bwana alipokuwa hawezi kuendelea kuvumilia matendo yenu maovu na mambo ya machukizo mliyoyafanya, nchi yenu ilikuwa kitu cha kulaania na kuachwa ukiwa pasipo wakazi, kama ilivyo leo.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.