Yeremia 44:1
Jeremiah 44:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Neno hili lilimjia Yeremia kuhusu Wayahudi wote waishio Misri, huko Migdoli, Tahpanhesi na Memfisi,* katika nchi ya Pathrosi* kusema:
Jeremiah 44:1 in English
Jeremiah 44:1 · Berean Standard Bible
This is the word that came to Jeremiah concerning all the Jews living in the land of Egypt *—in Migdol, Tahpanhes, and Memphis *—and in the land of Pathros:*
Context
1Neno hili lilimjia Yeremia kuhusu Wayahudi wote waishio Misri, huko Migdoli, Tahpanhesi na Memfisi,* katika nchi ya Pathrosi* kusema: 2“Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Mliona maangamizi makubwa niliyoyaleta juu ya Yerusalemu na juu ya miji yote ya Yuda. Leo imeachwa ukiwa na magofu 3kwa sababu ya uovu waliokuwa wameufanya. Walinikasirisha kwa kufukiza uvumba na kwa kuabudu miungu mingine ambayo kamwe wao, wala ninyi, wala baba zenu hawakuifahamu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.