Yeremia 42:3
Jeremiah 42:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Omba ili Bwana Mungu wako atuambie twende wapi na tufanye nini.”
Jeremiah 42:3 in English
Jeremiah 42:3 · Berean Standard Bible
Pray that the LORD your God will tell us the way we should walk and the thing we should do.”
Context
1Ndipo maafisa wote wa jeshi, pamoja na Yohanani mwana wa Karea, na Yezania mwana wa Hoshaya, na watu wote kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkuu sana wakamjia 2Yeremia nabii na kumwambia, “Tafadhali sikia maombi yetu na umwombe Bwana Mungu wako kwa ajili ya watu hawa wote waliosalia. Kwa kuwa kama unavyoona sasa, ingawa wakati fulani tulikuwa wengi, sasa tumesalia wachache tu. 3Omba ili Bwana Mungu wako atuambie twende wapi na tufanye nini.” 4Nabii Yeremia akajibu, “Nimewasikia. Kwa hakika nitamwomba Bwana Mungu wenu kama mlivyoomba. Nitawaambia kila kitu asemacho Bwana, wala sitawaficha chochote.” 5Kisha wakamwambia Yeremia, “Bwana na awe shahidi wa kweli na mwaminifu kati yetu kama hatutafanya sawasawa na kila kitu Bwana Mungu wako atakachokutuma utuambie.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.