Native Bible

Jeremiah 38:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yeremia akajibu, “Hawatakutia mikononi mwao. Mtii Bwana kwa kufanya kile ninachokuambia. Kisha utafanikiwa na maisha yako yatakuwa salama.

Jeremiah 38:20 in English

Jeremiah 38:20 · Berean Standard Bible

“They will not hand you over,” Jeremiah replied. “Obey the voice of the LORD in what I am telling you, that it may go well with you and you may live.

Context

18Lakini ikiwa hutajisalimisha kwa maafisa wa mfalme wa Babeli, mji huu utatiwa mikononi mwa Wakaldayo na watauteketeza kwa moto, nawe mwenyewe hutaweza kujiokoa mikononi mwao.’ ” 19Mfalme Sedekia akamwambia Yeremia, “Ninawaogopa Wayahudi ambao wamekimbilia kwa Wakaldayo, kwa kuwa Wakaldayo wanaweza kunitia mikononi mwao, nao wakanitenda vibaya.” 20Yeremia akajibu, “Hawatakutia mikononi mwao. Mtii Bwana kwa kufanya kile ninachokuambia. Kisha utafanikiwa na maisha yako yatakuwa salama. 21Lakini ukikataa kujisalimisha, hili ndilo Bwana alilonifunulia: 22Wanawake wote walioachwa katika jumba la kifalme la mfalme wa Yuda wataletwa mbele ya maafisa wa mfalme wa Babeli. Wanawake hao watakuambia: “ ‘Walikupotosha na kukushinda, wale rafiki zako uliowaamini. Miguu yako imezama matopeni; rafiki zako wamekuacha.’

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.