Native Bible

Jeremiah 35:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

wala kujenga nyumba za kuishi au kuwa na mashamba ya mizabibu, mashamba au mazao.

Jeremiah 35:9 in English

Jeremiah 35:9 · Berean Standard Bible

Nor have we built houses in which to live, and we have not owned any vineyards or fields or crops.

Context

7Pia msijenge nyumba kamwe, wala kuotesha mbegu au kupanda mashamba ya mizabibu. Kamwe msiwe na kitu chochote katika hivi, lakini siku zote lazima muishi kwenye mahema. Ndipo mtakapoishi kwa muda mrefu katika nchi ambayo ninyi ni wahamiaji.’ 8Tumetii kila kitu ambacho baba yetu Yonadabu mwana wa Rekabu alituamuru. Sisi wenyewe wala wake zetu wala wana wetu na binti zetu kamwe hatujanywa divai 9wala kujenga nyumba za kuishi au kuwa na mashamba ya mizabibu, mashamba au mazao. 10Tumeishi katika mahema na tumetii kikamilifu kila kitu alichotuamuru baba yetu Yonadabu. 11Lakini wakati Nebukadneza mfalme wa Babeli alipoivamia nchi hii, tulisema, ‘Njooni, lazima twende Yerusalemu ili kukimbia majeshi ya Wakaldayo na ya Washamu.’ Kwa hiyo tumeishi Yerusalemu.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.