Yeremia 33:18
Jeremiah 33:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
wala hata makuhani, ambao ni Walawi, kamwe hawatakosa mtu wa kusimama mbele zangu daima ili kutoa sadaka za kuteketezwa, ili kuteketeza sadaka ya nafaka na kutoa dhabihu.’ ”
Jeremiah 33:18 in English
Jeremiah 33:18 · Berean Standard Bible
nor will the priests who are Levites ever fail to have a man before Me to offer burnt offerings, to burn grain offerings, and to present sacrifices.”
Context
16Katika siku hizo, Yuda ataokolewa
na Yerusalemu ataishi salama.
Hili ndilo jina atakaloitwa:
Bwana Haki Yetu.’ 17Kwa maana hili ndilo asemalo Bwana: ‘Daudi kamwe hatakosa mtu wa kukalia kiti cha enzi cha nyumba ya Israeli, 18wala hata makuhani, ambao ni Walawi, kamwe hawatakosa mtu wa kusimama mbele zangu daima ili kutoa sadaka za kuteketezwa, ili kuteketeza sadaka ya nafaka na kutoa dhabihu.’ ” 19Neno la Bwana likamjia Yeremia kusema: 20“Hili ndilo asemalo Bwana: ‘Ikiwa mtaweza kuvunja agano langu kuhusu usiku na mchana, ili usiku na mchana visiwepo kwa nyakati zake,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.