Yeremia 29:9
Jeremiah 29:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wanawatabiria ninyi uongo kwa jina langu. Sikuwatuma,” asema Bwana.
Jeremiah 29:9 in English
Jeremiah 29:9 · Berean Standard Bible
For they are falsely prophesying to you in My name; I have not sent them, declares the LORD.”*
Context
7Pia tafuteni amani na mafanikio ya mji ambamo nimewapeleka uhamishoni. Mwombeni Bwana kwa ajili ya mji huo, kwa sababu ukistawi, ninyi pia mtastawi.” 8Naam, hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: “Msikubali manabii na wabashiri walioko miongoni mwenu wawadanganye. Msisikilize ndoto ambazo mmewatia moyo kuota. 9Wanawatabiria ninyi uongo kwa jina langu. Sikuwatuma,” asema Bwana. 10Hili ndilo asemalo Bwana: “Miaka sabini itakapotimia kwa ajili ya Babeli, nitakuja kwenu na kutimiza ahadi yangu ya rehema ya kuwarudisha mahali hapa. 11Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu,” asema Bwana, “ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.