Yeremia 25:17
Jeremiah 25:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hivyo nikakichukua kikombe kutoka mkononi mwa Bwana, na kuyafanya mataifa yote aliyonituma kwao kukinywa:
Jeremiah 25:17 in English
Jeremiah 25:17 · Berean Standard Bible
So I took the cup from the LORD’s hand and made all the nations drink from it, each one to whom the LORD had sent me,
Context
15Hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli, aliloniambia: “Chukua kutoka mkononi mwangu kikombe hiki kilichojaa divai ya ghadhabu yangu, na kuyanywesha mataifa yote ambayo ninakutuma kwao. 16Watakapoinywa, watapepesuka na kukasirika sana kwa sababu ya upanga nitakaoupeleka katikati yao.” 17Hivyo nikakichukua kikombe kutoka mkononi mwa Bwana, na kuyafanya mataifa yote aliyonituma kwao kukinywa: 18Yaani Yerusalemu na miji ya Yuda, wafalme wake na maafisa wake, kuwafanya magofu na kuwa kitu cha kuchukiza, cha dhihaka na laana, kama walivyo leo; 19pia Farao mfalme wa Misri, watumishi wake, maafisa wake na watu wake wote,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.