Yeremia 21:2
Jeremiah 21:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Tuulizie sasa kwa Bwana, kwa sababu Nebukadneza mfalme wa Babeli anatushambulia. Labda Bwana atatenda maajabu kwa ajili yetu kama nyakati zilizopita, ili Nebukadneza atuondokee.”
Jeremiah 21:2 in English
Jeremiah 21:2 · Berean Standard Bible
“Please inquire of the LORD on our behalf, since Nebuchadnezzar * king of Babylon is waging war against us. Perhaps the LORD will perform for us something like all His past wonders, so that Nebuchadnezzar will withdraw from us.”
Context
1Neno lilimjia Yeremia kutoka kwa Bwana wakati Mfalme Sedekia alipowatuma Pashuri mwana wa Malkiya, na kuhani Sefania mwana wa Maaseya kwake, kusema: 2“Tuulizie sasa kwa Bwana, kwa sababu Nebukadneza mfalme wa Babeli anatushambulia. Labda Bwana atatenda maajabu kwa ajili yetu kama nyakati zilizopita, ili Nebukadneza atuondokee.” 3Lakini Yeremia akawajibu, “Mwambieni Sedekia, 4‘Hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli, asemalo: Ninakaribia kuwageuzia silaha za vita zilizo mikononi mwenu, ambazo mnatumia kupigana na mfalme wa Babeli na Wakaldayo ambao wako nje ya ukuta wakiwazunguka kwa jeshi. Nami nitawakusanya ndani ya mji huu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.