Yeremia 20:8
Jeremiah 20:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kila ninenapo, ninapiga kelele nikitangaza ukatili na uharibifu. Kwa hiyo neno la Bwana limeniletea matukano na mashutumu mchana kutwa.
Jeremiah 20:8 in English
Jeremiah 20:8 · Berean Standard Bible
For whenever I speak, I cry out; I proclaim violence and destruction. For the word of the LORD has become to me a reproach and derision all day long.
Context
6Nawe Pashuri pamoja na wote waishio katika nyumba yako mtakwenda uhamishoni Babeli. Mtafia humo na kuzikwa, wewe na rafiki zako wote ambao umewatabiria uongo.’ ” 7Ee Bwana, umenidanganya,
nami nikadanganyika;
wewe una nguvu kuniliko,
nawe umenishinda.
Ninadharauliwa mchana kutwa,
kila mmoja ananidhihaki. 8Kila ninenapo, ninapiga kelele
nikitangaza ukatili na uharibifu.
Kwa hiyo neno la Bwana limeniletea matukano
na mashutumu mchana kutwa. 9Lakini kama nikisema, “Sitamtaja
wala kusema tena kwa jina lake,”
neno lake linawaka ndani ya moyo wangu kama moto,
moto uliofungwa ndani ya mifupa yangu.
Nimechoka sana kwa kulizuia ndani mwangu;
kweli, siwezi kujizuia. 10Ninasikia minongʼono mingi,
“Hofu iko pande zote!
Mshtakini! Twendeni tumshtaki!”
Rafiki zangu wote wananisubiri niteleze,
wakisema,
“Labda atadanganyika;
kisha tutamshinda
na kulipiza kisasi juu yake.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.