Yeremia 18:20
Jeremiah 18:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Je, mema yalipwe kwa mabaya? Lakini wao wamenichimbia shimo. Kumbuka kwamba nilisimama mbele yako na kunena mema kwa ajili yao, ili wewe ugeuze hasira yako kali mbali nao.
Jeremiah 18:20 in English
Jeremiah 18:20 · Berean Standard Bible
Should good be repaid with evil? Yet they have dug a pit for me. Remember how I stood before You to speak good on their behalf, to turn Your wrath from them.
Context
18Wakasema, “Njooni, tutunge hila dhidi ya Yeremia; kwa kuwa kufundisha sheria kwa kuhani hakutapotea, wala shauri litokalo kwa mwenye hekima, wala neno la manabii. Hivyo njooni, tumshambulie kwa ndimi zetu na tusijali chochote asemacho.” 19Nisikilize, Ee Bwana,
sikia wanayosema washtaki wangu! 20Je, mema yalipwe kwa mabaya?
Lakini wao wamenichimbia shimo.
Kumbuka kwamba nilisimama mbele yako
na kunena mema kwa ajili yao,
ili wewe ugeuze hasira yako kali mbali nao. 21Kwa hiyo uwaache watoto wao waone njaa;
uwaache wauawe kwa makali ya upanga.
Wake zao wasiwe na watoto, na wawe wajane;
waume wao wauawe,
nao vijana wao waume
wachinjwe kwa upanga vitani. 22Kilio na kisikike kutoka kwenye nyumba zao
ghafula uwaletapo adui dhidi yao,
kwa kuwa wamechimba shimo ili kunikamata
na wameitegea miguu yangu mitego.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.