Yeremia 17:16
Jeremiah 17:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sijakukimbia na kuacha kuwa mchungaji wako; unajua sijaitamani siku ya kukata tamaa. Kile kipitacho midomoni mwangu ki wazi mbele yako.
Jeremiah 17:16 in English
Jeremiah 17:16 · Berean Standard Bible
But I have not run away from being Your shepherd; I have not desired the day of despair. You know that the utterance of my lips was spoken in Your presence.
Context
14Uniponye, Ee Bwana, nami nitaponyeka;
uniokoe nami nitaokoka,
kwa maana wewe ndiwe ninayekusifu. 15Wao huendelea kuniambia,
“Liko wapi neno la Bwana?
Sasa na litimie!” 16Sijakukimbia na kuacha kuwa mchungaji wako;
unajua sijaitamani siku ya kukata tamaa.
Kile kipitacho midomoni mwangu
ki wazi mbele yako. 17Usiwe kwangu kitu cha kunitia hofu kuu;
wewe ndiwe kimbilio langu katika siku ya maafa. 18Watesi wangu na waaibishwe,
lakini nilinde mimi nisiaibike;
wao na watiwe hofu kuu,
lakini unilinde mimi na hofu kuu.
Waletee siku ya maafa;
waangamize kwa maangamizi maradufu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.