Yeremia 15:12
Jeremiah 15:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Je, mtu aweza kuvunja chuma, chuma kitokacho kaskazini, au shaba?
Jeremiah 15:12 in English
Jeremiah 15:12 · Berean Standard Bible
Can anyone smash iron— iron from the north—or bronze?
Context
10Ole wangu, mama yangu, kwamba ulinizaa,
mtu ambaye ulimwengu wote
unashindana na kugombana naye!
Sikukopa wala sikukopesha,
lakini kila mmoja ananilaani. 11Bwana akasema,
“Hakika nitakuokoa kwa kusudi jema,
hakika nitawafanya adui zako wakuombe msaada
nyakati za maafa na nyakati za dhiki. 12“Je, mtu aweza kuvunja chuma,
chuma kitokacho kaskazini, au shaba? 13Utajiri wako na hazina zako nitavitoa kuwa nyara,
bila gharama,
kwa sababu ya dhambi zako zote
katika nchi yako yote. 14Nitakufanya uwe mtumwa wa adui zako
katika nchi usiyoijua,
kwa kuwa katika hasira yangu moto umewashwa
utakaowaka juu yako daima.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.