Native Bible

Judges 9:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Lakini mzabibu ukaijibu, ‘Je, niache kutoa divai yangu inayofurahisha miungu na wanadamu ili nikawe juu ya miti?’

Judges 9:13 in English

Judges 9:13 · Berean Standard Bible

But the grapevine replied, ‘Should I stop giving my wine that cheers both God and man, to hold sway over the trees?’

Context

11“Lakini mtini ukaijibu, ‘Je, niache kutoa matunda yangu mazuri na matamu, ili niende nikawe juu ya miti?’ 12“Ndipo miti ikauambia mzabibu, ‘Njoo na uwe mfalme wetu.’ 13“Lakini mzabibu ukaijibu, ‘Je, niache kutoa divai yangu inayofurahisha miungu na wanadamu ili nikawe juu ya miti?’ 14“Mwishoni miti yote ikauambia mti wa miiba, ‘Njoo na uwe mfalme wetu.’ 15“Nao mti wa miiba ukaijibu, ‘Kama kweli mnataka niwe mfalme wenu, basi njooni mpate kupumzika chini ya kivuli changu. Lakini kama sivyo, moto na utoke kwenye mti wa miiba ukateketeze mierezi ya Lebanoni!’

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.