Waamuzi 8:17
Judges 8:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Pia akaubomoa mnara wa Penieli na kuwaua watu wa mji.
Judges 8:17 in English
Judges 8:17 · Berean Standard Bible
He also pulled down the tower of Penuel and killed the men of the city.
Context
15Ndipo Gideoni akaja na kuwaambia watu wa Sukothi, “Tazama, hapa wapo Zeba na Salmuna mlionisimanga kwa ajili yao mkisema, ‘Je, mikono ya Zeba na Salmuna tayari mnayo sasa ili tuweze kulipatia jeshi lako mikate?’ ” 16Akawachukua hao viongozi wa mji na kuwafundisha watu wa Sukothi somo kwa kuwaadhibu kwa miiba na michongoma ya nyikani. 17Pia akaubomoa mnara wa Penieli na kuwaua watu wa mji. 18Kisha akawauliza Zeba na Salmuna, “Ni watu wa aina gani mliowaua huko Tabori?”
Wakajibu, “Ni watu kama wewe, kila mmoja wao akiwa na nafasi ya uana wa mfalme.” 19Gideoni akajibu, “Hao walikuwa ndugu zangu, wana wa mama yangu hasa. Hakika kama aishivyo Bwana, kama mngekuwa mmewaacha hai, mimi nisingewaua ninyi.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.