Native Bible

Judges 6:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hivyo Gideoni akamjengea Bwana madhabahu mahali pale na kupaita, Yehova-Shalom.* Mpaka leo ingalipo imesimama huko Ofra ya Waabiezeri.

Judges 6:24 in English

Judges 6:24 · Berean Standard Bible

So Gideon built an altar to the LORD there and called it The LORD Is Peace.* To this day it stands in Ophrah of the Abiezrites.

Context

22Gideoni alipotambua kuwa ni malaika wa Bwana, akapiga kelele kwa mshangao, akasema, “Ole wangu, Bwana Mwenyezi! Kwa kuwa nimemwona malaika wa Bwana uso kwa uso!” 23Lakini Bwana akamwambia, “Amani iwe kwako! Usiogope. Hutakufa.” 24Hivyo Gideoni akamjengea Bwana madhabahu mahali pale na kupaita, Yehova-Shalom.* Mpaka leo ingalipo imesimama huko Ofra ya Waabiezeri. 25Usiku ule ule Bwana akamwambia, “Mchukue ngʼombe dume wa baba yako, yaani, yule wa pili mwenye miaka saba, na ubomoe madhabahu ya Baali aliyo nayo baba yako, na ukaikate Ashera iliyo karibu nayo. 26Kisha mjengee Bwana Mungu wako, madhabahu halisi, kwa taratibu zake, juu ya huu mwamba. Kwa kutumia kuni za hiyo nguzo ya Ashera uliyoikatakata, mtoe sadaka huyo dume wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.