Waamuzi 6:23
Judges 6:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini Bwana akamwambia, “Amani iwe kwako! Usiogope. Hutakufa.”
Judges 6:23 in English
Judges 6:23 · Berean Standard Bible
But the LORD said to him, “Peace be with you. Do not be afraid, for you will not die.”
Context
21Malaika wa Bwana akainyoosha fimbo iliyokuwa mkononi mwake, ncha yake ikagusa ile nyama na ile mikate isiyotiwa chachu, nao moto ukatoka kwenye mwamba ukateketeza ile nyama na ile mikate. Malaika wa Bwana akatoweka kutoka machoni pake. 22Gideoni alipotambua kuwa ni malaika wa Bwana, akapiga kelele kwa mshangao, akasema, “Ole wangu, Bwana Mwenyezi! Kwa kuwa nimemwona malaika wa Bwana uso kwa uso!” 23Lakini Bwana akamwambia, “Amani iwe kwako! Usiogope. Hutakufa.” 24Hivyo Gideoni akamjengea Bwana madhabahu mahali pale na kupaita, Yehova-Shalom.* Mpaka leo ingalipo imesimama huko Ofra ya Waabiezeri. 25Usiku ule ule Bwana akamwambia, “Mchukue ngʼombe dume wa baba yako, yaani, yule wa pili mwenye miaka saba, na ubomoe madhabahu ya Baali aliyo nayo baba yako, na ukaikate Ashera iliyo karibu nayo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.