Waamuzi 4:23
Judges 4:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Basi siku ile Mungu akamshinda Yabini, mfalme wa Kanaani, mbele ya Israeli.
Judges 4:23 in English
Judges 4:23 · Berean Standard Bible
On that day God subdued Jabin king of Canaan before the Israelites.
Context
21Ndipo Yaeli, mkewe Heberi, akatwaa kigingi cha hema, akachukua nyundo mkononi mwake, akamwendea polepole, akiwa amelala usingizi, akiwa amechoka. Akakigongomea kile kigingi kwenye paji la uso wake, kikapenya hata kuingia ardhini, naye akafa. 22Baraka akakaribia akimfuatia Sisera, Yaeli akatoka kumlaki. Akamwambia, “Njoo, nitakuonyesha mtu unayemtafuta.” Hivyo wakaingia ndani ya hema wakiwa wamefuatana na tazama Sisera alikuwa amelala humo, akiwa amekufa, na hicho kigingi cha hema kikiwa kimegongomewa kupitia paji la uso wake. 23Basi siku ile Mungu akamshinda Yabini, mfalme wa Kanaani, mbele ya Israeli. 24Nao mkono wa Waisraeli ukaendelea kuwa na nguvu zaidi na zaidi dhidi ya Yabini, mfalme wa Kanaani, mpaka wakamwangamiza.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.