Waamuzi 2:8
Judges 2:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Bwana, akafa akiwa na umri wa miaka 110.
Judges 2:8 in English
Judges 2:8 · Berean Standard Bible
And Joshua son of Nun, the servant of the LORD, died at the age of 110.
Context
6Baada ya Yoshua kuwapa watu ruhusa waende zao, Waisraeli wakaenda kwenye urithi wao wenyewe ili kumiliki nchi yao. 7Watu wakamtumikia Bwana siku zote za maisha ya Yoshua, na za hao wazee walioishi baada ya Yoshua kufa, waliokuwa wameona mambo makuu ambayo Bwana alikuwa ametenda kwa ajili ya Israeli. 8Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Bwana, akafa akiwa na umri wa miaka 110. 9Wakamzika katika nchi ya urithi wake, huko Timnath-Heresi* katika nchi ya vilima ya Efraimu, kaskazini ya Mlima Gaashi. 10Baada ya kizazi kile chote kukusanywa pamoja na baba zao, kikainuka kizazi kingine baada yao ambacho hakikumjua Bwana, wala matendo yale aliyokuwa ametenda kwa ajili ya Waisraeli.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.