Native Bible

Judges 2:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

kwa sababu walimwacha na kutumikia Baali na Maashtorethi.

Judges 2:13 in English

Judges 2:13 · Berean Standard Bible

for they forsook Him and served Baal and the Ashtoreths.

Context

11Kwa hiyo Waisraeli wakatenda maovu machoni pa Bwana na kuwatumikia Mabaali. 12Wakamwacha Bwana, Mungu wa baba zao, aliyekuwa amewatoa katika nchi ya Misri. Wakaifuata na kuiabudu miungu mbalimbali ya mataifa yanayowazunguka. Wakamkasirisha Bwana, 13kwa sababu walimwacha na kutumikia Baali na Maashtorethi. 14Hivyo hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia mikononi mwa wavamizi waliowateka nyara. Akawauza katika mikono ya adui zao pande zote, hivyo hawakuweza tena kuwazuia adui zao. 15Popote Israeli walipotoka kwenda kupigana, mkono wa Bwana ulikuwa kinyume nao ili kuwashinda, kama vile alivyokuwa amewaapia. Nao wakawa katika taabu kubwa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.