Waamuzi 13:22
Judges 13:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Manoa akamwambia mkewe, “Hakika tutakufa, kwa kuwa tumemwona Mungu.”
Judges 13:22 in English
Judges 13:22 · Berean Standard Bible
“We are going to die,” he said to his wife, “for we have seen God!”
Context
20Mwali wa moto kutoka hapo madhabahuni ulipowaka kuelekea mbinguni, malaika wa Bwana akapaa ndani ya huo mwali. Manoa na mkewe, kwa kuona jambo hili, wakaanguka chini kifudifudi. 21Malaika wa Bwana hakumtokea tena Manoa na mkewe. Ndipo Manoa akatambua kuwa huyo alikuwa malaika wa Bwana. 22Manoa akamwambia mkewe, “Hakika tutakufa, kwa kuwa tumemwona Mungu.” 23Lakini mkewe akamwambia, “Ikiwa Bwana alikuwa amekusudia kutuua, asingelipokea sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya unga kutoka mikononi mwetu, wala asingelituonyesha mambo haya yote wala kututangazia mambo kama haya wakati huu.” 24Yule mwanamke akazaa mtoto wa kiume akamwita jina lake Samsoni. Kijana akakua, naye Bwana akambariki.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.