Native Bible

Judges 11:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Basi Yefta akawakimbia ndugu zake akaenda kuishi katika nchi ya Tobu, mahali ambako watu waasi walijiunga naye na kumfuata.

Judges 11:3 in English

Judges 11:3 · Berean Standard Bible

So Jephthah fled from his brothers and settled in the land of Tob, where worthless men gathered around him and traveled with him.

Context

1Basi Yefta Mgileadi alikuwa mtu shujaa. Baba yake alikuwa Gileadi, naye mama yake alikuwa kahaba. 2Mke wa Gileadi akamzalia wana wengine, nao watoto hao walipokua, wakamfukuza Yefta na kumwambia, “Wewe huwezi kupata urithi katika jamii yetu, kwa sababu wewe ni mwana wa mwanamke mwingine.” 3Basi Yefta akawakimbia ndugu zake akaenda kuishi katika nchi ya Tobu, mahali ambako watu waasi walijiunga naye na kumfuata. 4Baada ya muda Waamoni wakafanya vita na Israeli, 5viongozi wa Gileadi wakaenda kumchukua Yefta katika nchi ya Tobu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.