Native Bible

Judges 11:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yefta akarudisha wajumbe kwa mfalme wa Waamoni,

Judges 11:14 in English

Judges 11:14 · Berean Standard Bible

Jephthah again sent messengers to the king of the Ammonites

Context

12Ndipo Yefta akatuma wajumbe kwa mfalme wa Waamoni akisema, “Una nini juu yetu, hata umekuja kushambulia nchi yetu?” 13Mfalme wa Waamoni akawajibu wajumbe wale wa Yefta, “Wakati Waisraeli walipopanda kutoka Misri, waliichukua nchi yangu kuanzia Arnoni mpaka Yaboki, hadi kufikia Yordani. Sasa rudisha kwa amani.” 14Yefta akarudisha wajumbe kwa mfalme wa Waamoni, 15kusema: “Hili ndilo asemalo Yefta, Israeli hawakuchukua nchi ya Moabu wala ya Waamoni. 16Lakini walipopanda kutoka Misri, Israeli walipitia katika jangwa hadi Bahari ya Shamu na wakafika Kadeshi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.